Alhamisi 24 Septemba 2026 - 08:05
Heshima ya Kudumu ya Wananchi Watiifu kwa Madhehebu na Nafasi ya Marji' wa Shia/ Qum Yamuaga Kihistoria Kielelezo cha Fiqhi na Maadili

Wananchi na wanazuoni wa dini wa mji mtakatifu wa Qom, ambao ni makao ya Ahlul-Bayt wa Mtume (saww), leo kwa mara nyingine wamethibitisha ni kwa kiasi gani wanawapenda na kuvutiwa na wanazuoni na maraji' wa taqlidi, ambao ni nguzo za elimu ya fiqhi, imani, maadili na dini.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, bila shaka hata kama siku ya Jumatano, Serikali na Ofisi ya Gavana wa Qom isingetangaza likizo rasmi, bado tungeshuhudia umati mkubwa na wa kushangaza katika sherehe za kuusindikiza mwili mtakatifu wa Ayatullah al-Udhma Sayyid Musa Shubayri Zanjani.

Jambo hili lenyewe kwa mara nyingine linathibitisha kwamba wananchi watiifu wa mji mtakatifu wa Qom, ambao ni makao ya Ahlul-Bayt wa Muhammad (as), pamoja na wananchi wa maeneo mengine, ni wenye mapenzi makubwa na shauku kwa wanazuoni na maraji' wa taqlidi, ambao ni nguzo za elimu ya fiqhi, imani, maadili na dini.

Tukio kubwa lililovuka mipaka ya mazishi ya kawaida

Ingawa muda rasmi wa kuanza hafla hiyo ilitangazwa kuwa saa 9:00 asubuhi, lakini takribani saa moja kabla, makundi ya wananchi waliovaa mavazi meusi, hususan wanazuoni wa dini na wanafunzi wa masomo ya Hawza, walikuwa tayari wamekusanyika katika maeneo yanayouzunguka Uwanja wa Jihad wa Qom. Hivyo, baada ya idadi ya watu kuongezeka zaidi, hafla ya kuusindikiza mwili iilianza.

Uwepo wa umati mkubwa wa waumini wenye hamasa, hususan watu wa elimu na maarifa, katika tukio hili la kiroho, uliunda tena tukio kubwa la maombolezo kutokana na kufariki Marji' wa Kishia, na ukaonesha kwamba hafla kama hizi zinazidi kuwa zaidi ya mazishi ya kawaida, na kuwa dhihirisho la uhusiano wa kina kati ya uongozi wa kidini wa Marjaiya na wananchi wote wenye dini.

Uwepo mkubwa wa wanazuoni na viongozi wa dini katika kumuaga Marji' wa Taqlidi

Kwa upande mwingine, safu zilizoendelea za nyuso mashuhuri kutoka Hawza mbalimbali, wakiwa wamevaa mavazi ya kidini na kuonesha heshima iliyochanganyika na huzuni na majonzi kutokana na kufariki mmoja wa viongozi wakubwa wa wanazuoni wa dini, zimetuma ujumbe wa umoja na mwendelezo wa njia ya Marjaiya kwenye jamii. Uwepo huu wenyewe unakumbusha kwamba mfumo wa fiqhi wa marehemu Ayatullah al-Udhma Shubayri Zanjani ni urithi ambao umejikita miongoni mwa vizazi mbalimbali vya wanazuoni wa dini na unaendelea kurithishwa.

Hali ya umati wa watu jana ilikuwa kwa hakika mchanganyiko wa majonzi na huzuni iliyosababishwa na kumpoteza mwalimu mkubwa na mwanazuoni mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, pamoja na faraja inayopatikana kwa kukumbuka fadhila, sifa njema na uchamungu wake.

Katika maeneo mbalimbali ya hafla hiyo, mashairi ya kutoa pole kwa Imam Mahdi (aj) kutokana na msiba huu yalisomwa. Na bila shaka, kama ilivyo katika mazishi yote ya wanazuoni na watu mashuhuri, kusomwa kwa maombolezo ya Sayyid al-Shuhadaa Imam Hussein (as) na Hadhrat Fatimah al-Zahra (sa) kuliyapamba mazishi haya ya heshima, aidha ilionekana wazi kusomwa nyimbo za maombolezo za kuomboleza kutokuwepo kwa Mwenye Amri (aj) na waimbaji wa Ahlul-Bayt (as). Sambamba na hayo, kupepea bendera zilizopambwa majina ya Maasumu (as), pamoja na bendera takatifu ya nchi yetu na pia bendera nyekundu yenye maandishi ya “Ya Litha'rat al-Hussein (as)”, katika njia ndefu iliyopitiwa na waombolezaji, kulilipa tukio hili mwonekano wa kipekee.

Heshima ya Kudumu ya Wananchi Watiifu kwa Madhehebu na Nafasi ya Marji' wa Shia/ Qum Yamuaga Kihistoria Kielelezo cha Fiqhi na Maadili

Nyota ang'avu katika anga ya fiqhi na dini

Katikati ya umati huo, macho yangu yalimuona mwanazuoni mmoja wa dini ninayemfahamu. Ni mwalimu mwenye ulemavu ambaye nilipata fursa ya kuwa mwanafunzi wake kwa miaka kadhaa katika taaluma ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Qom. Hujjatul-Islam wal-Muslimin Adel Sarikhani, mhadhiri wa Chuo Kikuu hicho, katika mazungumzo mafupi, huku akitoa salamu za rambirambi kwa kifo cha mwanazuoni huyu mkubwa na faqihi mashuhuri wa Hawza, alisema: “Marehemu Ayatullah Shubayri Zanjani alikuwa na historia kubwa na rekodi ya kuvutia katika uwanja wa kuzalisha elimu za Hawza na kueneza maarifa ya Ahlul-Bayt (as). Yeye mwenyewe alinufaika na masomo kutoka kwa wanazuoni wakubwa kama vile Ayatullah al-Udhma Borujerdi, Ayatullah al-Udhma Khoei na Muhaqqiq Damad. Kwa miaka mingi, katika uwanja wa utafiti na uchunguzi, pamoja na ufundishaji na malezi ya wanafunzi wengi, kwa hakika alituachia urithi muhimu wa utamaduni wa fiqhi na misingi ya elimu ya kidini uliosimama juu ya misingi halisi ya Hawza.”

Aliongeza: “Yeye alikuwa, kwa maana halisi ya neno, miongoni mwa nyota ang’avu za fiqhi, misingi ya fiqhi, elimu ya kalamu na elimu ya wapokezi wa hadithi katika Hawza. Kwa kutegemea hazina ya elimu, uchamungu, ikhlasi na maadili, alitembea katika njia ya kuuongoza umati wa waumini. Bila shaka, kifo chake kimeacha pengo kubwa katika mwili wa kielimu wa Shia na katika ulimwengu wa Kiislamu, na kuziba pengo hili kutapatikana tu kwa kuendeleza njia yake ya kielimu na kimaadili.”

Kielelezo bora katika njia ya kujifunza na kueneza elimu za Ahlul-Bayt (as)

Katika kuendelea na safari hiyo adhimu ya mazishi, kabla ya kufika kwenye makutano ya Barabara ya Sokoni, nilizungumza na mmoja wa wanafunzi vijana wa Hawza aliyekuwepo katika hiyo hizlyo. Nilimuuliza: “Kwa maoni yako, ni siri gani ya umaarufu na kudumu wanazuoni na watu wakubwa kama marehemu Ayatullah al-Udhma Shubayri?”

Alijibu: “Kwa hakika, mimi ambaye ni mwanafunzi wa daraja la sita katika Hawza, sikupata fursa ya kuhudhuria darsa za Marji' huyu wa taqlidi aliyekuwa mcha Mungu na mwenye hadhi kubwa, lakini nimekuwa nikisikia sifa zake njema kutoka kwa walimu wetu wengi, miongoni mwa mambo niliyoyasikia ni kwamba, pamoja na kuwa na uchamungu, kujiepusha na mambo ya shubha na unyenyekevu mkubwa, alikuwa mtu mwenye umakini mkubwa wa kielimu. Katika kufafanua masuala ya fiqhi na misingi ya fiqhi, alikuwa akijitahidi kuhakikisha kwamba jambo linaeleweka vizuri kwa wanafunzi na wanazuoni, badala ya kuyapita masuala hayo kwa juu juu.”

Heshima ya Kudumu ya Wananchi Watiifu kwa Madhehebu na Nafasi ya Marji' wa Shia/ Qum Yamuaga Kihistoria Kielelezo cha Fiqhi na Maadili

Aliongeza: “Binafsi ninaamini kwamba, mbali na mwenendo na mtindo wa maisha yake, kazi za kielimu alizoacha Marji' huyu aliyefariki ni kumbukumbu bora kwa watu wote wa elimu na wale wote ambao wameweka moyo wao katika kueneza maarifa ya Qur’ani na Ahlul-Bayt. Watu hawa wakubwa, kupitia mtindo wao wa maisha ya kielimu, yenye ikhlasi na wakati huo huo ya unyenyekevu na kutoridhika na anasa, wakifuata mfano wa Maasumina (as), ni vielelezo bora kwa watu wetu, hususan wanafunzi na wanazuoni wa Hawza.”

Uchambuzi kutoka kwa Sayyid Muhamad Mahd Mousavi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha